Wednesday, May 26, 2010

BOYS WILL ALWAYS BE BOYS







Hii kweli kali kishenzi hivi jamani kweli kunawanaume wa stahili hii? picha kwa hisani ya www.learnshareandinspire.blogspot.com











Friday, February 12, 2010

We! unafikiri kiinglishi ni mchezo








Jamani tucfanye mchezo na hii lugha wewe ona mpaka wenyewe wanaboronga.

Happy Valentine to you

Jamani napenda kuwaambia kuwa nawapenda wote mnaonipenda na pia napenda kuwatakia Valentine njema wote

Tuesday, February 2, 2010

Paka Anayedaiwa Kuwa na Uwezo wa Kunusa Kifo Kabla Hakijatokea

Ukimuona ni paka wa kawaida ambaye hana tofauti yoyote na paka wengine lakini inasemwa kuwa ana uwezo wa kuwatambua wagonjwa wanaokaribia kufariki hospitalini na hadi sasa imesemwa kuwa ameishafanikiwa kuvinusa vifo vya wagonjwa 50 kabla hata havijatokea
Paka anayejulikana kwa jina la Oscar hujisogeza na kukaa karibu na kitanda cha mgonjwa aliyebakiza muda mchache kufariki.Iwapo ndugu wa mgonjwa huyo watamfukuza paka huyo nje ya chumba cha mgonjwa wao na kumfungia mlango, basi paka huyo hugoma kuondoka na huanza kuukwaruza mlango kwa nguvu aking'ang'ania kuingia ndani.Paka Oscar ambaye huishi katika nyumba moja ya kutunza wagonjwa wazee iliyopo kwenye mji wa Province katika jimbo la Rhode Island nchini Marekani hupenda kuzungukazunguka toka chumba kimoja hadi kingine katika nyumba hiyo.Inadaiwa kuwa Paka Oscar huwa hapendi kutumia muda wake pamoja na vikongwe katika nyumba hiyo isipokuwa wale tu ambao wanakaribia kufariki.Tabia ya paka huyo ambaye hivi sasa ana umri wa miaka mitano, iligunduliwa mwaka 2007 na manesi wa nyumba hiyo ambao kwa jinsi walivyo na uhakika na uwezo wa paka Oscar huwataarifu familia ya mgonjwa anayezungukiwa sana na paka huyo kuwa mambo yanaelekea kuwa mabaya.Katika kuonyesha uwezo wa paka huyo, siku moja manesi walimchukua paka huyo na kumweka kwenye kitanda cha mgonjwa ambaye waliamini atafariki dakika yoyote ile, lakini paka huyo alichoropoka na kukimbilia chumba cha pili yake.Uamuzi wa paka Oscar ulijionyesha siku hiyo hiyo kwa mgonjwa wa chumba cha pili kufariki siku hiyo hiyo jioni wakati mgonjwa wa chumba cha kwanza aliendelea kuishi kwa angalau siku mbili kabla ya kufariki paka Oscar akiwa amerudi pembeni ya kitanda chake.Wataalamu hivi sasa wanamfanyia uchunguzi paka huyo ambaye alianza kulelewa kwenye hospitali hiyo tangia alipokuwa kichanga.Mmmoja wa wanasayansi anayemfanyia uchunguzi paka huyo, Dr David Dosa, ameelezea mshangao wake kwa uwezo wa paka huyo kutabiri bila kukosea vifo vya wagonjwa 50 katika kipindi cha miaka mitano.Dokta Dosa anasema kuwa hakuna maelezo yoyote ya kisayansi kuelezea tabia ya paka huyo.Katika tukio jingine, mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina la Richards aliamua kukaa pembeni ya kitanda cha mama yake muda wote baada ya madaktari kumwambia kuwa mama yake aliyekuwa mgonjwa mahututi angefariki muda wowote ule.Richard bila kupumzika alikaa pembeni ya kitanda cha mama yake kwa siku tatu mfululizo lakini mama yake hakufariki.Madaktari walimshauri Richard aende nyumbani kwake akapumzike kidogo kabla ya kurudi baadae. Richard kwa shingo upande alikubali kuondoka kwenda kwake kupumzika.Muda mfupi baada ya kuondoka, mama yake alifariki. Hakufariki akiwa peke yake bali Oscar alikuwa pembeni yake.

Tuesday, January 26, 2010

JK Atoa tamko kuhusu miundombinu kutengenezwa haraka

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka kutengeneza upya miundombinu nchini, hasa reli na barabara, iliyoharibiwa kutokana na mvua na mafuriko ya wiki za karibuni katika baadhi ya mikoa nchini.Mheshimiwa Rais pia amehimiza ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za kiraia na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kukabiliana na kazi ya kukarabati miundombinu hiyo.“Uchumi huu utaishiwa sana nguvu kama hatukushughulikia haraka suala la kukarabati miundombuni na hasa reli,” Rais Kikwete amekiambia kikao cha dharura alichokiitisha mchana wa leo, Jumatatu, Januari 25, 2010, Ikulu, Dar es Salaam, kujadili kiwango cha uharibifu na jinsi ya kunusuru miundombinu ya reli na barabara.Rais Kikwete aliagiza kufanyika kwa kikao hicho Ijumaa iliyopita, Januari 22, 2010, wakati alipoendesha kikao cha Baraza la Mawaziri.Waziri wa Miundombinu, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa amewaongoza maofisa waandamizi kutoka wizara yake na kutoka baadhi ya makampuni na mashirika yaliyoko chini ya wizara yake, ikiwamo Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Wakala wa Barabara (Tanroads) katika kikao cha leo.Katika kikao hicho, maofisa hao walimweleza Rais Kikwete uharibifu uliofanyika katika Reli ya Kati na hasa kati ya Stesheni za Gulwe na Kilosa, katika mikoa ya Dodoma na Morogoro, kutokana na mvua zilizonyesha katika wilaya za Mpwapwa na Kilosa kati ya Desemba 24, mwaka jana, 2009 na Januari 10, mwaka huu, 2010.Katika maeneo ya Kilosa, mvua hizo na mafuriko yaliyoandamana na mvua hizo, yameng’oa kabisa sehemu ya Reli ya Kati na kusimamisha huduma za reli hiyo kati ya Dar es Salaam na Dodoma.Sababu kubwa za uharibifu huo ni kufurika na kwa mito ya Mkondoa na Kinyasungwi, hali iliyosababisha kuhama kwa mito hiyo kutoka katika njia za asili na kuelekea kwenye tuta la reli.Maofisa hao wamemweleza Rais Kikwete kuwa zipo sehemu 28 zilizoharibika kati ya stesheni hizo mbili lakini ni sehemu 26 zilizoaharibika zaidi. Pia wamemweleza kuwa madaraja tisa yamesombwa na maji na mengine matatu yako katika hatari ya kusombwa.Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mhandisi Omar Chambo pia amemweleza Rais Kikwete mipango ya ukarabati wa sehemu hiyo ya reli na kuahidi kuwa kazi hiyo inaweza kuwa imekamilika kati ya miezi miwili na miezi mitatu.Kuhusu uharibifu kwenye barabara, Mhandisi Chambo amesema kuwa uharibufu kwenye barabara umefanyika katika mikoa 18 ya Tanzania Bara.Mikoa hiyo ni Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Kigoma, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Singida, Tabora na Tanga.Mhandisi Chambo amesema kuwa kiasi cha sh bilioni 13.286 zinahitajika kuweza kukarabati barabara hizo ambazo zimeharibika kwa viwango tofauti huku uharibifu mkubwa ukiwa umetokea katika Mkoa wa Dodoma ambako barabara zake tatu hazipitiki.Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,DAR ES SALAAM.25 Januari, 2010

Kweli tumetoka mbali

yani tumetoka mbali tangu enzi za makari ya chupa za maji na matairi ndio vifuniko vyake mpaka sasa tuna bofya kwenye ma computer ni balaa

New style

Hivi naomba kuuliza kwamba hii style ikianzishwa kwa hapa tanzania tutaweza au?

Kama mambo yenyewe ndiyo haya!


Mh! kama mambo yenyewe ya kuwa gado ndo haya mimi siyataki, hapo kwenye picha inaonyesha jinsi mafunzo ya kuwa gado yanavyo anza mimi binafsi naona kabla ya kufanya hayo mazoezi hutakiwi kula chochote mpaka kwanza umalize coz unaweza ukashtukia umetapika chakula chote ulicho kula na hata kwa wakati mwingine una weza uka sababisha hali ya hewa kuchafuka au siyo jamani.

Hivi ulishawahi kuwa na mawazo?


Jamani Bull Dog sijui anawaza nini na cjui kwanini amekuwa hivyo? labda wadau mnisaidie