Thursday, December 31, 2009

Mzee Kawawa afariki dunia leo


WAZIRI Mkuu wa za zamani, Mzee Rashidi Mfaume Kawawa 'Simba wa vita' amefariki dunia leo asubuhi.
Mzee Kawawa alikuwa ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, MWalimu Julius Kambarage Nyerere.Kawawa amefariki dunia leo asubuhi,31,Desember, 2009, akiwa na umri wa miaka 83.Kwa habari kamili juu ya kifo na historia kamili ya waziri mkuu huyo kitawajia punde.Mungu ailaze roho ya marehemu peponi Amina

Tuesday, December 29, 2009

Tanzania bila ukimwi inawezekana kweli au?


IMEDAIWA kuwa ndani ya miezi mitatu kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu watu wapatao 4072 wameambukizwa virusi vya ukimwi katika Manispaa ya Kionodnoni jijini Dar es Salaam
Hayo yalijulikana baada ya kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Manispaa hiyo kutoa takwimu hiyo.Kati ya watu hao, 1,165 ni wanaume na 2,911 ni wanawake ambapo wote walipewa rufaa kwenda katika vituo vya kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU nchini.Katika taarifa iliyotolea na kamati hiyo imesema watu hao wataanza tiba ya huduma ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU na katika Manispaa hiyo kuna jumla ya vituo 17 vya kupata vidonge hivyo.Imesema kwa sasa katika vituo hivyo wameshafikia wagonjwa 12,829 ambao wamejiandikisha.Pia taarifa hiyo ilidai kuwa kwa sasa wagonjwa wanaotumia dawa hizo ARVs ni 7,033 huku wengine wakiendelea na huduma za uchunguzi na ufuatiliaji na endapo CD4 zitashuka chini ya 200 wataanzishiwa dawa.Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa manispaa imetenga kiasi cha Shilingi. milioni 109.9 ili kuimarisha vita dhidi ya kuenea ugonjwa huo katika kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Julai mwakani.

Tuesday, December 8, 2009

MIAKA 48 YA UHURU KESHO

Ama kwa hakika kesho tuna kwenda kusheherekea miaka 48 ya uhuru ivyo nawatakia watanzania wote siku njema ya kesho na iwe ya amani na usalama kwa wote kwani na hakika kila mmoja atakuwa na uhuru wa kufanya jambo analolitarajia kwa kesho, mimi, wewe, na yule tusikose kukutana pale katika uwanja wa uhuru kuanzia saa 06:00 asubui Lango litakuwa wazi kwaajili ya wanchi kuingia na kuweza kushuhudia kwa umakini kwa kinachoendelea.

Monday, December 7, 2009

Umaga afariki dunia




MCHEZA mieleka maarufu duniani, Eki “Eddie” Fatu ambaye anajulikana kwa jina la “Umaga” amefariki Ijumaa iliyopita huko Houston, Marekani, kutokana na shambulio la moyo.Kifo cha mwanamichezo huyo, kimeongeza orodha ya wacheza mieleka wa kulipwa ambao wamefariki wakiwa hawajafikia umri wa miaka 40.

Fatu, aliyekuwa na umri wa miaka 36, na ambaye alipata umaarufu mkubwa hivi karibuni katika medani ya mieleka chini ya chama cha World Wrestling Entertainment (WWE) akitumia jina la “Umaga,” alikutwa na mkewe akiwa amezimia katika chumba chake huko Spring, Texas, na hivyo akamkimbiza hospitali.
Umaga alipatwa na shambulio jingine la pili la moyo akiwa hospitalini hapo na akafariki.

Fatu, mtu ambaye alikuwa anafahamika kutokana na michoro (tattoo) iliyokuwa usoni mwake, anatoka katika familia kubwa ya wapigana mieleka wa Samoa ambao wameifanya biashara ya mchezo huo kuwa maarufu kwa vizazi kadhaa.

Umaarufu wao ulianzia kwa baba zake wadogo, Afa na Sika Anoi’a, ambao walijulikana katika medani hiyo kama “Wasamoa wa Msituni” (The Wild Samoans) mnamo miaka ya 1970 na 1980.

Mtu maarufu zaidi katika ukoo huo alikuwa ni binamu yake aliyeitwa Dwayne “The Rock” Johnson, ambaye aliacha mieleka na kujikita katika medani ya filamu huko Hollywood.

Kilele cha mafanikio ya Fatu kilikuwa mwaka 2007 aliposhiriki tamasha la Wrestlemania 23 huko Detroit ambalo liliwapa umaarufu mkubwa, mmiliki wa WWE, Vince McMahon na Donald Trump.

Hata hivyo, umaarufu wake ulikuwa wa muda mfupi na aliondolewa katika mkataba wa WWE tarehe 8 Juni alipokataa kwenda katika kituo cha huduma ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kwenda kinyume na sera ya matumizi ya madawa hayo kwa mujibu wa WWE.

Ni hivi karibuni tu alikuwa amerejea katika ziara binafsi ya maonyesho ya mieleka aliyoifanya Australia ambapo alikumbwa na tatizo hilo ambalo liliondoa uhai wake.

“Kwa niaba ya familia yangu, familia ya Anoa’i na Fatu, tumesikitishwa na kushitushwa na kifo cha Eki wetu,” Afa Anoa’i aliliambia gazeti la Wrestling Obeserver.

“Kwetu alikuwa ni mtoto, binamu, kaka, mume, na baba yetu. Mioyo yetu imekumbwa na simanzi na hakuna maneno yanayoweza kuelezea hisia zetu. Ni jambo la faraja kufahamu Eki alivyopendwa na familia yake, watu wa rika lake, marafiki na wapenzi wake wote.”

Idadi kubwa ya wacheza mieleka vijana wamekufa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, na kuwafanya baadhi yao kuamini kwamba mchezo huo una laana.

Miongoni mwa matukio mabaya zaidi yalimhusisha Chris Benoit (40) ambaye alijiua huko Georgia mwaka 2007 baada ya kumwua mkwe, Nancy, na mwanaye Daniel.

Mwingine ni Eddie Guerrero (38) aliyekufa kwa shambulio la moyo mwaka 2005 huko Minnesota katika hoteli moja.
Mcheza mieleka Owen Hart (33) naye alikufa huko Kansas City mwaka 1999 baada ya kuumia katika onyesho lililokuwa likichukuliwa na televisheni.

Vilevile, mnamo Machi mwaka huu, mcheza mieleka mwingine wa zamani wa WWE, Andrew “Test” Martin (34), alifariki kwa kutumia kiwango kikubwa zaidi cha madawa ya Oxycontin.

Thursday, December 3, 2009

Christmas hiyo inanukia tena kwa kasi




Jamani yani sasa hivi tunahesabu siku tu ili tuweze kuifikia siku kuu ya krismas pamoja na kuusherekea mwakampya kinachotakiwa ni kuomba afya njema na uzima kutoka kwa Mungu baba mwenyezi aliye hai juu mbinguni, vilevile najua shamra shamra za mapambo ndani yanyumba ni kama kawaida, kama vile miti ya Christmas pamoja na mengine mengi.

USINYWE RED BULL -- NI HATARI KWA MAISHA YAKO – HASA VIJANA


RED BULL Huuzwa katika maduka makubwa (Supermarkets) na madogo (Retail Shops) katika nchi ya Tanzania na watu wazima na watoto wetu wengi wana mazoea ya kunywa kinywaji hiki ambacho kinaweza kusababisha kifo! Kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha RED BULL zilitengenezwa maalum katika maabara za kijeshi za Marekani kwa ajili ya kutuliza mzuka wa maaskari wao wakati wakitekeleza mauaji ya kikatili sana dhidi ya wananchi wa Vietnam miaka ya sitini na sabini. Kemikali hizo zilitumika pia kama dawa ya kuwazindua watu waliozirai (“stress coma”).Hazikukusudiwa kutumiwa kama kinywaji au kilevi cha kawaida!

kwa habari zaidi waono Globalpublishers.