IMEDAIWA kuwa ndani ya miezi mitatu kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu watu wapatao 4072 wameambukizwa virusi vya ukimwi katika Manispaa ya Kionodnoni jijini Dar es Salaam
Hayo yalijulikana baada ya kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Manispaa hiyo kutoa takwimu hiyo.Kati ya watu hao, 1,165 ni wanaume na 2,911 ni wanawake ambapo wote walipewa rufaa kwenda katika vituo vya kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU nchini.Katika taarifa iliyotolea na kamati hiyo imesema watu hao wataanza tiba ya huduma ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU na katika Manispaa hiyo kuna jumla ya vituo 17 vya kupata vidonge hivyo.Imesema kwa sasa katika vituo hivyo wameshafikia wagonjwa 12,829 ambao wamejiandikisha.Pia taarifa hiyo ilidai kuwa kwa sasa wagonjwa wanaotumia dawa hizo ARVs ni 7,033 huku wengine wakiendelea na huduma za uchunguzi na ufuatiliaji na endapo CD4 zitashuka chini ya 200 wataanzishiwa dawa.Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa manispaa imetenga kiasi cha Shilingi. milioni 109.9 ili kuimarisha vita dhidi ya kuenea ugonjwa huo katika kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Julai mwakani.
No comments:
Post a Comment