Saturday, June 27, 2009

Enjoy yyour weekend

hey, just wish u a gud weekend
Cheers!

Thursday, June 25, 2009

Michael Jackson afariki dunia


Michael Jackson one of pop music's biggest stars, has died after reportedly suffering a heart attack.
EARLY LIFE:
Jackson was born on Aug. 29, 1958, in Gary, Indiana, the seventh of nine children. Five Jackson boys - Jackie, Tito, Jermaine, Marlon and Michael - first performed together at a talent show when Michael was 6. They walked off with first prize.
Their group later became The Jackson Five, and when it was signed by Motown Records in the late 1960s it underwent its final metamorphosis to become The Jackson 5. Jackson made his first solo album in 1972.
SUCCESS: Jackson released "Thriller" in 1982, which became a smash hit that yielded seven top-ten singles. The album sold 21 million copies in the United States and at least 27 million worldwide.
The next year, he unveiled his signature "moonwalk" dance move while performing "Billie Jean" during an NBC special.
Jackson's lifetime record sales tally is believed to be about 750 million, which, added to the 13 Grammy Awards he has received, makes him one of the most successful entertainers of all time.
ACCUSATIONS In 1993, Jackson was accused of sexually abusing a 13-year-old boy, and police raided his California ranch "Neverland".
The same year, Jackson announced he had become addicted to painkillers and abruptly canceled a world tour to promote his album, "Dangerous."
He reached a settlement in 1994, later reported to be $23m with the family of the boy he was accused of abusing.
MARRIAGE & FAMILY: In 1994, Jackson married Elvis Presley's only child, Lisa Marie, but the marriage ended in divorce in 1996. Jackson married Debbie Rowe the same year and had two children, before splitting in 1999. The couple never lived together.
Jackson has three children named Prince Michael I, Paris Michael and Prince Michael II, known for his brief public appearance when his father held him over the railing of a hote balcony, causing widespread criticism.
MORE CONTROVERSY: A television documentary "Living with Michael Jackson" was screened in 2003, saying that Jackson still had sleepovers with young boys and had his third child with a surrogate mother. Jackson aired his own rebuttal.
Jackson went on trial in 2005 on charges of molesting a 13-year-old boy in 2003, as well as conspiring to abduct the boy. The singer faced nearly 20 years in prison if convicted.
The four-month trial ended in June 2005 with his being acquitted of all charges. Jackson has spent time in Bahrain, Ireland and France since then.
COMEBACK? After several false dawns, Jackson and music promoter AEG Live announced he would perform 50 concerts at London's O2 Arena. Jackson had been due to start the concerts on July 13.
Jackson had been rehearsing in the Los Angeles area for the London shows, which sold out within hours of within hours of going on sale in March.

Hatariiiiiiiiiiii!

hizo ndiyo faida za ufugaji wa mbwa ndani yanyumba jamaa kajiona kajifiiiicha wakati mbwa ali muona sasa anamuumbua

Vitu vingine bwana!

Sasa ninge wapa kamtiani kwamba uniambie kinachofuata hapo nini ? na uhakika ningepata majibu mengi tena tofauti sana na kilichopo au siyo?

Qeen Doreen huyooooooo! ndani ya game kwa mara ya pili

Msanii mdogo wa Bongo Falava ambae sio mgeni sana masikioni mwa wengi amerudi tena, ni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, Aliamua amalizie masomo yake ya Sekondari kwanza na sasa amerudi... Amekua kiakili hata kimwili sio mdogo mdogo tena kama zamani na anaonekana mrembo zaidi....Single yake mpya inayoitwa "NAMTESA" itaanza kusikika redioni hivi karibuni na kuonekana kwenye televisheni mbali mbali...Huyo ndio Queen Doreen Bwana

Umewahi kuona?



Ushawahi kuona ndege ikisimama kwenye mataa ya barabarani ili kupisha magari yapite na yenyewe ipite wakati inapopaa au kutua kwenye uwanja wa ndege? Uwanja wa ndege huo haupatikani kokote duniani zaidi ya nchi ndogo ya Gibraltar ambayo ipo chini ya utawala wa Uingereza. Kwa habari kamili kuhusiana na uwanja huo wa ndege link ni hii:www.nifahamishe.com/
Wapi Haleluya aongee kitumaana huyu mdau jamani ameniambia yeye amewahi kuona ndege inayo kimbia kuliko mwanga wa taa zake! jamani hiyo ipo kweli au mnakubaliana nayo?

Wednesday, June 24, 2009

Pombe mbaya jamani

Hivi kwa nini binadamu tunapenda pombe kiasi cha kuhatarisha afya zetu?
Mtu kama huyu unamsaidiaje? maana hapo hasikii maumivu ngoja pombe ziishe kichwani sijui atamlilia nani

Usidharau kazi jamani


Eti tuna sema tuna kazi ngumu embu cheki huyo kazi yake ni ngumu au rahisi kushinda yako?

Mtetezi wa Mkapa

Na John Daniel, DodomaMBUNGE wa Kwela Dkt. ChrisantMzindakaya, (CCM) amemtetea Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akisema wanaomtuhumu kuwa hakuwa kiongozi mzuri hawana hoja kwa vile alifanya mambo mengi mazuri kwa manufaa ya taifa.Amewataka Wabunge wenzake ambao alidai wanampiga vita Bw. MKapa, kutambua kuwa chuki na kumwandamana mtu nao pia ni ufisadi.Akichangi bajeti ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa Bungeni juzi, Mbunge huyo alisema wabunge wanzake wanapima ufisadi kwa fedha badala ya roho zao na kuongeza kwamba kufanya hivyo ni kosa kwa kuwa kinachotakiwa ni mtu kupima roho yake kwanza kama ni safi kabla ya kumjadili mwingine kwa kigezo cha fedha.“Binadamu ana kasoro moja kubwa sana ya kutazama ubaya kuliko mazuri 10, hapa nitanukuu Biblia Yoshua 5:15 na sura ya 6:4. “Usiwe fisadi katika jambo kubwa wala dogo, wala usipite kuwa adui badala ya rafiki roho ya ufisadi itamharibu yeye aliye na nayo hata kumfanya mzaha kwa adui zake”' alisema.Mbunge huyo aliisifia Serikaliya Rais Jakaya Kikwete kwa kutaja baadhi ya mafanikio katika nyanja za elimu, miundo mbinu ya barabara na afya na kuwataka wabunge watambue kwamba Serikali ya awamu ya nne ni nzuri na imetoka kwa Mungu.“Serikali hii nzuri imetoka wapi kama si kwa Mungu, hii Serikali imetoka kwa Mungu, hata hizi lawama anazopata Rais Mkapa, ni za Shetani tu, hivi kweli kwa miaka 10 hakuna alichofanya,“?alihoji Dkt. Mzindakaya.Kwa upande wake, Mbunge wa Kilindi Bi.Beatrice Shellukindo, (CCM), alilalamikia utendaji wa baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali kwa kuchelewesha maamuzi huku akitaka kampeni chafu zinazoendeshwa na baadhi ya mawaziri wanaowania majimbo yaUchaguzi mwaka 2010 zikomeshwe.Alisema mmoja wa mawaziri wa sasaalifika jimboni kwake na kufanya kampeni chafu na kuongeza kwamba yeye kama Mbunge hakatai mtu kufanya kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwakani lakini ni lazima anayetaka kufanya hivyo afuate taratibuzilizopo na kusisitiza kuwa hakuna mtu mwenye hati miliki ya Jimbo.

JK awataka wakulima wakubwa kuwasaidia wakulima wadogo

Rais Jakaya Kikwete, amewataka wakulima wakubwa nchini kuwasaidia kwa ujuzi na nyenzo nyingine, wakulima wadogo wanaozunguka mashamba ya wakulima wakubwa hao.
Aidha, Rais Kikwete amesema Serikali yake inawakaribisha kwa mikono miwili wakulima wakubwa ambao wanaweza kuisaidia Tanzania kujitosheleza kwa chakula na hata kuzalisha akiba ya kuweza kuuza nje.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu, jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa kampuni ya Capricon Investment Group, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake, Ion Yadigaroglu.
Kampuni hiyo imeanza kulima mpunga na maharage katika Bonde la Mto Kilombero, Mkoani Morogoro, ikiwa inashirikiana kupitia ubia na Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (Rubada).
Mwaka huu, kampuni hiyo imelima kiasi cha hekta 2,000 na inalenga kuzalisha kiasi cha tani 20,000 za mpunga kila mwaka. Tanzania inahitaji kiasi cha tani 100,000 za mchele kwa sasa kwa mwaka ili kujitosheleza kwa aina hiyo ya nafaka.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alimwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake tayari imewekeza kiasi cha dola za Marekani milioni 20, na inakusudia kuwekeza zaidi katika kilimo cha mazao hayo mawili.
Rais Kikwete ameishukuru kampuni hiyo kwa kuonyesha imani na kuwekeza katika kilimo cha Tanzania na ameitaka kuimarisha uhusiano kati yake na wakulima wadogo wenye mashamba yanayozungumza shamba la kampuni hiyo.
Hata hivyo, Rais alisema ni hamu yake kuona wakulima wakubwa wanaowekeza katika kilimo cha Tanzania wakiwasaidia wakulima wadogo wanaozunguka mashamba yao kwa namna ya kuongezea tija, ubora na uzalishaji wakulima hao wadogo.
“Hawa wakulima wadogo wanaweza kuwa wabia na washirika wenu muhimu. Mnaweza kuboresha ujuzi wao kwa kuwapa mafunzo ya kilimo cha kisasa. Mnaweza kuwafanya wakulima bora wa mpunga, mnaweza kuhamisha sehemu ya ujuzi wenu kwenda kwao, mnaweza kununua mpunga toka kwao, mnaweza kushirikiana nao kwa kujaribu matokeo ya tafiti mbali mbali mpya za kilimo,” alisema Rais Kikwete.
Kampuni hiyo inakusudia kukiuza hapa hapa nchini chakula chote ambacho itakilima nchini na haitaanza kuuza nje hadi itakapokuwa imetoshelezaji mahitaji ya ndani ya nchi.
Vile vile, Rais Kikwete ameahidi kuisaidia kampuni hiyo kukabiliana na baadhi ya changamoto zake kama vile kuboresha barabara kutoka kwenye shamba la kampuni hiyo hadi mjini Ifakara, umbali wa karibuni kilomita 80.


Mama Salma Kikwete na Mama Anna Mkapa

Mwenyekiti wa mfuko wa wanawake na maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa mfuko wa fursa kwa wote (EOTF) mama Mkapa wakiagana baada ya semina ya wanawake wajasiriamali kufunguliwa na Rais wa Zanzibar katika ukumbi wa Chuo cha uhasibu Kurasini. Picha kwa hisani ya Ikulu.

Bungeni

Wabunge wa wamechacha katika kikao cha Bunge kinachoendelea, kila mmoja analalama, wengine wanashutumu mawaziri kwa kuwabania. wamewasha moto sijui mambo yatakuaje katika mabunge yanayofuata.Mbunge wa Mchinga, Mudhihil kamshukia ndugu yake wa Mkoa wa Lindi, Bernard Membe kwamba anafanya mtimanyongo ili kiwanda cha Saruji kisijengwe katika jimbo lake. Membe ni wa Mtama hukohuko Lindi.AkasemaKuna waziri ana hindaskama nyoka wa mdimu, hali ndimu wala majani yake, lakini mtu akitaka kuchuma anambania. Akaongeza kuwa hatamtaja, lakini akasisitiza kuwa Kondoo wa Manyoya atazizima mwenyewe na kujitokeza hadharani.Ana hamu ya urais mwaka 2015.Jana, Membe kasema kuwa suala hilo linamuhusu yeye kwa hivyo atachukua hatua za kichama chao! Mambo hayo.Beatrice Shelukindo nae katoa mpya anasema kuna waziri anajipitisha jimbo la Kilindi. Na kusema kuwa watendaji wamekuwa na ugonjwa wa kufanya mambo kama watakavyo na kudai kuwa serikali inaumwa inahitaji mambo ya masheikh na wachungaji!Mzindakaya nae akaibuka na kusema kuwa wabunge wa CCM watembee kifua mbele kwa kujivunia maendeleo walioletea wananchi. Mbunge huyo ambaye amedumu ndani ya jumba kubwa pengine kuliko asilimia 99 ya wabunge waliopo, alisema kuwa kwa mmiaka yote aliyokuwamo huko,wabunge wa sasa ndio wamefanya kazi zaidi tokea uhuru! Mambo hayoSijui tunaelekea wapi, ama Uchaguzi unakaribia?

Ajali Mbeya

Ajali sasa zimekuwa kiboko maisha yanapotea kila kukicha kam ahili fuso lilivyosababisha vifo vya watu saba Mbeya na kujeruhiwa wengine 40. Mabasi noma, malori noma vibajaji ndio kabisaa!! pikipiki wauaji kibao sasa Sijui tutatumia usafiri gani hii hali ikiendelea!

Mazishi ya Nasma Khamisi

Mwili wa marehemu ukifukiwa
Mumewe Omari Akimuombea Dua Marehemu mkewe

MWili wa marehemu Nasma ukielekea makaburini tayari kwa kuzikwa


Umati wa watu ulifurika Kumuaga Marehemu Nasma





















Tuesday, June 23, 2009

HAPO CHACHA

Mimi na wewe tu
Na haya ni mambo ya Cheers

NASMA KHAMIS KIDOGO AFARIKI DUNIA

Habari za kusikitisha zilizotufikia asubuhi zinasema kuwa Mwimbaji maarufu wa taarabu nchini Tanzania, Nasma Khamis Kidogo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na anatarajiwa kuzikwa kesho jijini Dar. Marehemu alijipatia umaarufu mkubwa katika ulimwengu wa Taarabu. Habari zaidi juu ya kifo chake zitawajia kupitia magaeti yetu yajayo. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi - Amin

Monday, June 22, 2009

Ni chakula pamoja na maliasili
















































Hicho ni chakula cha wenzetu kikiwa Sokoni na Matayarishoni.







Saturday, June 20, 2009

Friday, June 19, 2009

MMLIKI WA ZEUTAMU AKAMATWA

Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa(Interpol),wamefani kiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye anaasili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wamiaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu. NduguMalecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wakompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahil ina kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana nawenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupataushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idaraya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzaniamjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo naAmos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee JobLusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali zautumishi wa serikali Nchini Tanzania.Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwaTanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwaunadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumuudhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huoulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali yaTanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri yaMuungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada yapicha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini niwazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania. Licha ya Ndg. MalecelaPolisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katikamiji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani, ambao pia wanahusishwana Mtandao huo wa Ze Utamu.

Thursday, June 18, 2009

VIJIMAMBO VYA KATUNI


BALOZI MPYA WA MAREKANI

Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania,
Mh Alfonso Lenhardt

Rais Obama amteua Alfonso Lenhardt (pichani) kuwa Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaRais Barack Obama amemteua Mheshimiwa Alfonso E. Lenhardt kuwa Balozi wake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa mfumo unaotumiwa na Serikali ya Marekani, Rais huteua Mabalozi kwa mashauriano na hatimaye kupata ridhaa ya Bunge la Seneti la Marekani.Toka Mwezi Mei 2004, Mheshimiwa Lenhardt amekuwa Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Kuzuia Uhalifu (National Crime Prevention Council - NCPC) ambalo ni taasisi isiyo ya Kiserikali na isiyozalisha faida. Pia alikuwa Makamu wa Rais wa Kundi la Makampuni ya Shaw akishughulikia Uhusiano na Serikali.
Tarehe 4 Septemba 2001 aliteuliwa kuwa Mpambe wa Bunge (Sergeant-at-Arms) wa 36 wa Bunge la Seneti la Marekani na kuwa Muamerika wa Kwanza mwenye asili ya Kiafrika kuhudumu katika wadhifa huo ndani ya Bunge la Marekani. Aidha, alihudumu kama Makamu wa Rais na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Baraza linaloshughulikia Wakfu Mbalimbali (Council on Foundations).
Mheshimiwa Lenhardt alistaafu kutoka katika Jeshi la Marekani hapo August 1997 akiwa na cheo cha Meja Jenerali, baada ya kulitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 30 katika ngazi mbalimbali za uongozi.
Wadhifa wake wa mwisho jeshini ulikuwa ni Mkuu wa Kamandi ya Uajiri, yenye makao makuu yake huko,Fort Knox, KY, ambao aliongoza na kusimamia taasisi iliyojumuisha zaidi ya watu 13,000 waliokuwa katika zaidi ya vituo vya kazi 1,800.
Aidha, aliwahi kudumu kama Afisa Mwandamizi wa Polisi Jeshi (Senior Military Police Officer) katika oparesheni zote za kipolisi na masuala ya usalama katika Jeshi la Marekani sehemu mbalimbali duniani.
Mheshimiwa Lenhardt ambaye alizaliwa katika jiji la New York ni mtu wa nondozzz kisawasawa. Ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Sheria kuhusu Makosa ya Jinai kutoka katika Chuo Kikuu cha Nebraska, Shahada ya Pili ya Sanaa Katika Utawala kutoka katika Chuo Kikuu cha Central Michigan na Shahada ya Pili ya Sayansi ya Utawala katika Sheria kutoka katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Wichita.
Aidha, Mheshimiwa Lenhardt ni mhitimu wa awamu ya 94 Katika Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Usalama cha FBI; programu ya Viongozi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai ya Jeshi la Marekani . Aidha ni mhitimu wa Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Kivita (the National War College) na Chuo Kikuu cha Mambo ya Kijeshi na Usalama (National Defence University).
Kuhusu Uteuzi wa Mheshimiwa Lenhardt na mabalozi wengine, Rais Obama alisema, "Wamarekani watafaidika sana kwa kuwa na watumishi hawa waliotukuka, wake kwa waume, kama wawakilishi wao nchi za nje.
Vipaji, uzoefu na kujitoa kwao kikamilifu kutakuwa na mchango mkubwa sana tunapoendelea kuimarisha ubia kati ya Marekani na mataifa mbalimbali duniani kote na kukabiliana na changamoto kubwa za karne ya 21.
Ninashukuru kwa utumishi wao na nina shauku kubwa ya kufanya kazi na kila mmoja wao."Kwa taarifa zaidi kuhusu tangazo la uteuzi huu kutoka Ikulu ya Marekani tembelea tovuti:
http://www.whitehouse.gov/the_press_
office/President-Obama-Announces-More-
Key-Administration-Posts-6-11-09/

VIJIMAMBO

Haya sasa paka yeye kaamua kurekebisha saa
Na hawa nao wanamngojea mwenye gari wamuulize kwanini kapaki kwenye imaya yao?


Hapo chacha element imepata mvaaji sasa sijui trafiki atasemaje akimkamata

New Blog

Haya jamani na mimi najaribu libeneke la Kublog