Rais Jakaya Kikwete, amewataka wakulima wakubwa nchini kuwasaidia kwa ujuzi na nyenzo nyingine, wakulima wadogo wanaozunguka mashamba ya wakulima wakubwa hao.
Aidha, Rais Kikwete amesema Serikali yake inawakaribisha kwa mikono miwili wakulima wakubwa ambao wanaweza kuisaidia Tanzania kujitosheleza kwa chakula na hata kuzalisha akiba ya kuweza kuuza nje.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu, jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa kampuni ya Capricon Investment Group, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake, Ion Yadigaroglu.
Kampuni hiyo imeanza kulima mpunga na maharage katika Bonde la Mto Kilombero, Mkoani Morogoro, ikiwa inashirikiana kupitia ubia na Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (Rubada).
Mwaka huu, kampuni hiyo imelima kiasi cha hekta 2,000 na inalenga kuzalisha kiasi cha tani 20,000 za mpunga kila mwaka. Tanzania inahitaji kiasi cha tani 100,000 za mchele kwa sasa kwa mwaka ili kujitosheleza kwa aina hiyo ya nafaka.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alimwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake tayari imewekeza kiasi cha dola za Marekani milioni 20, na inakusudia kuwekeza zaidi katika kilimo cha mazao hayo mawili.
Rais Kikwete ameishukuru kampuni hiyo kwa kuonyesha imani na kuwekeza katika kilimo cha Tanzania na ameitaka kuimarisha uhusiano kati yake na wakulima wadogo wenye mashamba yanayozungumza shamba la kampuni hiyo.
Hata hivyo, Rais alisema ni hamu yake kuona wakulima wakubwa wanaowekeza katika kilimo cha Tanzania wakiwasaidia wakulima wadogo wanaozunguka mashamba yao kwa namna ya kuongezea tija, ubora na uzalishaji wakulima hao wadogo.
“Hawa wakulima wadogo wanaweza kuwa wabia na washirika wenu muhimu. Mnaweza kuboresha ujuzi wao kwa kuwapa mafunzo ya kilimo cha kisasa. Mnaweza kuwafanya wakulima bora wa mpunga, mnaweza kuhamisha sehemu ya ujuzi wenu kwenda kwao, mnaweza kununua mpunga toka kwao, mnaweza kushirikiana nao kwa kujaribu matokeo ya tafiti mbali mbali mpya za kilimo,” alisema Rais Kikwete.
Kampuni hiyo inakusudia kukiuza hapa hapa nchini chakula chote ambacho itakilima nchini na haitaanza kuuza nje hadi itakapokuwa imetoshelezaji mahitaji ya ndani ya nchi.
Vile vile, Rais Kikwete ameahidi kuisaidia kampuni hiyo kukabiliana na baadhi ya changamoto zake kama vile kuboresha barabara kutoka kwenye shamba la kampuni hiyo hadi mjini Ifakara, umbali wa karibuni kilomita 80.

No comments:
Post a Comment