Na John Daniel, DodomaMBUNGE wa Kwela Dkt. ChrisantMzindakaya, (CCM) amemtetea Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akisema wanaomtuhumu kuwa hakuwa kiongozi mzuri hawana hoja kwa vile alifanya mambo mengi mazuri kwa manufaa ya taifa.Amewataka Wabunge wenzake ambao alidai wanampiga vita Bw. MKapa, kutambua kuwa chuki na kumwandamana mtu nao pia ni ufisadi.Akichangi bajeti ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa Bungeni juzi, Mbunge huyo alisema wabunge wanzake wanapima ufisadi kwa fedha badala ya roho zao na kuongeza kwamba kufanya hivyo ni kosa kwa kuwa kinachotakiwa ni mtu kupima roho yake kwanza kama ni safi kabla ya kumjadili mwingine kwa kigezo cha fedha.“Binadamu ana kasoro moja kubwa sana ya kutazama ubaya kuliko mazuri 10, hapa nitanukuu Biblia Yoshua 5:15 na sura ya 6:4. “Usiwe fisadi katika jambo kubwa wala dogo, wala usipite kuwa adui badala ya rafiki roho ya ufisadi itamharibu yeye aliye na nayo hata kumfanya mzaha kwa adui zake”' alisema.Mbunge huyo aliisifia Serikaliya Rais Jakaya Kikwete kwa kutaja baadhi ya mafanikio katika nyanja za elimu, miundo mbinu ya barabara na afya na kuwataka wabunge watambue kwamba Serikali ya awamu ya nne ni nzuri na imetoka kwa Mungu.“Serikali hii nzuri imetoka wapi kama si kwa Mungu, hii Serikali imetoka kwa Mungu, hata hizi lawama anazopata Rais Mkapa, ni za Shetani tu, hivi kweli kwa miaka 10 hakuna alichofanya,“?alihoji Dkt. Mzindakaya.Kwa upande wake, Mbunge wa Kilindi Bi.Beatrice Shellukindo, (CCM), alilalamikia utendaji wa baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali kwa kuchelewesha maamuzi huku akitaka kampeni chafu zinazoendeshwa na baadhi ya mawaziri wanaowania majimbo yaUchaguzi mwaka 2010 zikomeshwe.Alisema mmoja wa mawaziri wa sasaalifika jimboni kwake na kufanya kampeni chafu na kuongeza kwamba yeye kama Mbunge hakatai mtu kufanya kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwakani lakini ni lazima anayetaka kufanya hivyo afuate taratibuzilizopo na kusisitiza kuwa hakuna mtu mwenye hati miliki ya Jimbo.
RAIS MWINYI:SERIKALI INAJIPANGA UJENZI WA MAGHALA YA CHAKULA
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi
ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa Ujenzi wa Maghala ya Kuhifadhia
Chakula...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment