Friday, June 19, 2009

MMLIKI WA ZEUTAMU AKAMATWA

Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa(Interpol),wamefani kiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye anaasili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wamiaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu. NduguMalecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wakompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahil ina kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana nawenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupataushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idaraya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzaniamjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo naAmos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee JobLusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali zautumishi wa serikali Nchini Tanzania.Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwaTanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwaunadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumuudhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huoulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali yaTanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri yaMuungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada yapicha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini niwazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania. Licha ya Ndg. MalecelaPolisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katikamiji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani, ambao pia wanahusishwana Mtandao huo wa Ze Utamu.

No comments:

Post a Comment