Mwimbaji mahiri wa muziki wa nyimbo za kiroho alias injili nchini,Jennifer Mgendi anatarajia kuizindua albamu yake ya sita itakayoitwa Kiu ya Nafsi itakayozinduliwa Novemba 29 katika ukumbi wa Landmark Hotel jijini.
kwa taarifa aliyoitoa hivi karibuni,Jennifer alisema kuwa albamu yake itakuwa na jumla ya nyimbo 10,aidha akabainisha kuwa uzinduzi huo utashirikisha wanamuziki mbalimbali watakaompa tafu katika uzinduzi wake.
Jennifer alizitaja baadhi ya nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo kuwa ni pamoja na jaribu Langu,Kutapambazuka,Nitasubiri Fadhili,Unifundishe kusifu na nyinginezo.
Aidha jennifer amewataja baadhi ya wanamuziki watakaosindikiza uzinduzi wake kuwa ni Upendo Nkone,Cosmas Chidumule,Charles Jangalason,Neema Mwaipopo,Cristina Mwan'gonda,Ann Annie,The Wispes band,Trinity Band pamoja na Wema sanga.
Jennifer alisema kuwa katika onesho hili la kiroho kutakuwepo na kiingilio ambacho kimepangwa kuwani shilingi 3000/= kwa watu wazima na watoto watalipa shilingi 2000/= na kwa viti maalum itakuwa ni shilingi 10,000/=.
Albamu alizowahi kuzindua hapo awali ni pamoja na na Nini aliyoitoa mnamo mwaka 1995,Ukarimu wake (2000),Nikiona Fahari (2001), Yesu Nakupenda (2002) pamoja na albamu ya Mchimba Mashimo aliyoitoa mnamo mwaka 2006.
Aidha pamoja na kupata mafanikio kwa namna moja ama nyingine katika fani ya uimbaji wanyimbo za Injili,Jennifer pia amewahi kutoa filamu kadhaa hapo awali ambayo ni Joto la roho, Pigo la faraja, teke la Mama na nyinginezo .
No comments:
Post a Comment