Thursday, December 31, 2009

Mzee Kawawa afariki dunia leo


WAZIRI Mkuu wa za zamani, Mzee Rashidi Mfaume Kawawa 'Simba wa vita' amefariki dunia leo asubuhi.
Mzee Kawawa alikuwa ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, MWalimu Julius Kambarage Nyerere.Kawawa amefariki dunia leo asubuhi,31,Desember, 2009, akiwa na umri wa miaka 83.Kwa habari kamili juu ya kifo na historia kamili ya waziri mkuu huyo kitawajia punde.Mungu ailaze roho ya marehemu peponi Amina

Tuesday, December 29, 2009

Tanzania bila ukimwi inawezekana kweli au?


IMEDAIWA kuwa ndani ya miezi mitatu kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu watu wapatao 4072 wameambukizwa virusi vya ukimwi katika Manispaa ya Kionodnoni jijini Dar es Salaam
Hayo yalijulikana baada ya kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Manispaa hiyo kutoa takwimu hiyo.Kati ya watu hao, 1,165 ni wanaume na 2,911 ni wanawake ambapo wote walipewa rufaa kwenda katika vituo vya kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU nchini.Katika taarifa iliyotolea na kamati hiyo imesema watu hao wataanza tiba ya huduma ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU na katika Manispaa hiyo kuna jumla ya vituo 17 vya kupata vidonge hivyo.Imesema kwa sasa katika vituo hivyo wameshafikia wagonjwa 12,829 ambao wamejiandikisha.Pia taarifa hiyo ilidai kuwa kwa sasa wagonjwa wanaotumia dawa hizo ARVs ni 7,033 huku wengine wakiendelea na huduma za uchunguzi na ufuatiliaji na endapo CD4 zitashuka chini ya 200 wataanzishiwa dawa.Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa manispaa imetenga kiasi cha Shilingi. milioni 109.9 ili kuimarisha vita dhidi ya kuenea ugonjwa huo katika kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Julai mwakani.

Tuesday, December 8, 2009

MIAKA 48 YA UHURU KESHO

Ama kwa hakika kesho tuna kwenda kusheherekea miaka 48 ya uhuru ivyo nawatakia watanzania wote siku njema ya kesho na iwe ya amani na usalama kwa wote kwani na hakika kila mmoja atakuwa na uhuru wa kufanya jambo analolitarajia kwa kesho, mimi, wewe, na yule tusikose kukutana pale katika uwanja wa uhuru kuanzia saa 06:00 asubui Lango litakuwa wazi kwaajili ya wanchi kuingia na kuweza kushuhudia kwa umakini kwa kinachoendelea.

Monday, December 7, 2009

Umaga afariki dunia




MCHEZA mieleka maarufu duniani, Eki “Eddie” Fatu ambaye anajulikana kwa jina la “Umaga” amefariki Ijumaa iliyopita huko Houston, Marekani, kutokana na shambulio la moyo.Kifo cha mwanamichezo huyo, kimeongeza orodha ya wacheza mieleka wa kulipwa ambao wamefariki wakiwa hawajafikia umri wa miaka 40.

Fatu, aliyekuwa na umri wa miaka 36, na ambaye alipata umaarufu mkubwa hivi karibuni katika medani ya mieleka chini ya chama cha World Wrestling Entertainment (WWE) akitumia jina la “Umaga,” alikutwa na mkewe akiwa amezimia katika chumba chake huko Spring, Texas, na hivyo akamkimbiza hospitali.
Umaga alipatwa na shambulio jingine la pili la moyo akiwa hospitalini hapo na akafariki.

Fatu, mtu ambaye alikuwa anafahamika kutokana na michoro (tattoo) iliyokuwa usoni mwake, anatoka katika familia kubwa ya wapigana mieleka wa Samoa ambao wameifanya biashara ya mchezo huo kuwa maarufu kwa vizazi kadhaa.

Umaarufu wao ulianzia kwa baba zake wadogo, Afa na Sika Anoi’a, ambao walijulikana katika medani hiyo kama “Wasamoa wa Msituni” (The Wild Samoans) mnamo miaka ya 1970 na 1980.

Mtu maarufu zaidi katika ukoo huo alikuwa ni binamu yake aliyeitwa Dwayne “The Rock” Johnson, ambaye aliacha mieleka na kujikita katika medani ya filamu huko Hollywood.

Kilele cha mafanikio ya Fatu kilikuwa mwaka 2007 aliposhiriki tamasha la Wrestlemania 23 huko Detroit ambalo liliwapa umaarufu mkubwa, mmiliki wa WWE, Vince McMahon na Donald Trump.

Hata hivyo, umaarufu wake ulikuwa wa muda mfupi na aliondolewa katika mkataba wa WWE tarehe 8 Juni alipokataa kwenda katika kituo cha huduma ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kwenda kinyume na sera ya matumizi ya madawa hayo kwa mujibu wa WWE.

Ni hivi karibuni tu alikuwa amerejea katika ziara binafsi ya maonyesho ya mieleka aliyoifanya Australia ambapo alikumbwa na tatizo hilo ambalo liliondoa uhai wake.

“Kwa niaba ya familia yangu, familia ya Anoa’i na Fatu, tumesikitishwa na kushitushwa na kifo cha Eki wetu,” Afa Anoa’i aliliambia gazeti la Wrestling Obeserver.

“Kwetu alikuwa ni mtoto, binamu, kaka, mume, na baba yetu. Mioyo yetu imekumbwa na simanzi na hakuna maneno yanayoweza kuelezea hisia zetu. Ni jambo la faraja kufahamu Eki alivyopendwa na familia yake, watu wa rika lake, marafiki na wapenzi wake wote.”

Idadi kubwa ya wacheza mieleka vijana wamekufa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, na kuwafanya baadhi yao kuamini kwamba mchezo huo una laana.

Miongoni mwa matukio mabaya zaidi yalimhusisha Chris Benoit (40) ambaye alijiua huko Georgia mwaka 2007 baada ya kumwua mkwe, Nancy, na mwanaye Daniel.

Mwingine ni Eddie Guerrero (38) aliyekufa kwa shambulio la moyo mwaka 2005 huko Minnesota katika hoteli moja.
Mcheza mieleka Owen Hart (33) naye alikufa huko Kansas City mwaka 1999 baada ya kuumia katika onyesho lililokuwa likichukuliwa na televisheni.

Vilevile, mnamo Machi mwaka huu, mcheza mieleka mwingine wa zamani wa WWE, Andrew “Test” Martin (34), alifariki kwa kutumia kiwango kikubwa zaidi cha madawa ya Oxycontin.

Thursday, December 3, 2009

Christmas hiyo inanukia tena kwa kasi




Jamani yani sasa hivi tunahesabu siku tu ili tuweze kuifikia siku kuu ya krismas pamoja na kuusherekea mwakampya kinachotakiwa ni kuomba afya njema na uzima kutoka kwa Mungu baba mwenyezi aliye hai juu mbinguni, vilevile najua shamra shamra za mapambo ndani yanyumba ni kama kawaida, kama vile miti ya Christmas pamoja na mengine mengi.

USINYWE RED BULL -- NI HATARI KWA MAISHA YAKO – HASA VIJANA


RED BULL Huuzwa katika maduka makubwa (Supermarkets) na madogo (Retail Shops) katika nchi ya Tanzania na watu wazima na watoto wetu wengi wana mazoea ya kunywa kinywaji hiki ambacho kinaweza kusababisha kifo! Kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha RED BULL zilitengenezwa maalum katika maabara za kijeshi za Marekani kwa ajili ya kutuliza mzuka wa maaskari wao wakati wakitekeleza mauaji ya kikatili sana dhidi ya wananchi wa Vietnam miaka ya sitini na sabini. Kemikali hizo zilitumika pia kama dawa ya kuwazindua watu waliozirai (“stress coma”).Hazikukusudiwa kutumiwa kama kinywaji au kilevi cha kawaida!

kwa habari zaidi waono Globalpublishers.

Friday, November 27, 2009

Eid Njema



Ingawaje waswali suni wamesheherekea leo sikukuu tukufu ya Eid, waislamu wengine wanakwenda kusheherekea sikukuu hiyo hapo kesho hivyo nawatakia sikukuu njema natumuombe Allah ipite kwa Amani kabisaaaaaaaaa.

Wednesday, November 25, 2009

Jennifer Mgendi kuzindua Albam mpya ya kiu ya Nafsi



Mwimbaji mahiri wa muziki wa nyimbo za kiroho alias injili nchini,Jennifer Mgendi anatarajia kuizindua albamu yake ya sita itakayoitwa Kiu ya Nafsi itakayozinduliwa Novemba 29 katika ukumbi wa Landmark Hotel jijini.

kwa taarifa aliyoitoa hivi karibuni,Jennifer alisema kuwa albamu yake itakuwa na jumla ya nyimbo 10,aidha akabainisha kuwa uzinduzi huo utashirikisha wanamuziki mbalimbali watakaompa tafu katika uzinduzi wake.

Jennifer alizitaja baadhi ya nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo kuwa ni pamoja na jaribu Langu,Kutapambazuka,Nitasubiri Fadhili,Unifundishe kusifu na nyinginezo.

Aidha jennifer amewataja baadhi ya wanamuziki watakaosindikiza uzinduzi wake kuwa ni Upendo Nkone,Cosmas Chidumule,Charles Jangalason,Neema Mwaipopo,Cristina Mwan'gonda,Ann Annie,The Wispes band,Trinity Band pamoja na Wema sanga.

Jennifer alisema kuwa katika onesho hili la kiroho kutakuwepo na kiingilio ambacho kimepangwa kuwani shilingi 3000/= kwa watu wazima na watoto watalipa shilingi 2000/= na kwa viti maalum itakuwa ni shilingi 10,000/=.

Albamu alizowahi kuzindua hapo awali ni pamoja na na Nini aliyoitoa mnamo mwaka 1995,Ukarimu wake (2000),Nikiona Fahari (2001), Yesu Nakupenda (2002) pamoja na albamu ya Mchimba Mashimo aliyoitoa mnamo mwaka 2006.


Aidha pamoja na kupata mafanikio kwa namna moja ama nyingine katika fani ya uimbaji wanyimbo za Injili,Jennifer pia amewahi kutoa filamu kadhaa hapo awali ambayo ni Joto la roho, Pigo la faraja, teke la Mama na nyinginezo .

Tuesday, November 24, 2009

Kumbe hata bendera ya Man U ilipeperushwa







Bendera ya Man U ilipopeperushwa na mkali Chidbenzi ndani ya Fiesta One Love katika Viwanja vya Posta.

Friday, November 20, 2009

Enjoy your week end guys



sasa ngoja tuone safari hii itakuwaje kwa hawa wakali wa ligi maana kesho anakwenda kuki hapenisha na Everton.

Thursday, November 12, 2009

Internet na vioja vyake

kupata mchumba c lazima uwe kijana hata wazee pia hupata kupitia internet.

NEW FASHION SHOES



fashion mpya ya viatu imeingia wahi sasa ujipatie size yako kwani viko vichache sana kama unavihitaji unaweza kuwasiliana na wahusika, wahi sasa bei ni nafuu kabisaaaaaaaaaaaaaaa! chaguo lako tu.

Wednesday, November 11, 2009

R.Kelly Kutembelea wahanga Vietnam

King wa R&B duniani Robert Sylvester Kelly "R. Kelly" mapema wiki hii kupitia mtandao wake ametangaza kuwa anajiandaa kuitembelea Nchi ya Vietnam kwa ajili ya kusaidia na kutoa msaada kwa wahanga wa mafuriko yaliyoikumba Nchi hiyo hivi juzi kati.
R.Kelly amesema amesikitishwa na vifo vingi vya watoto vilivyotokea wakati wa mafuriko hayo na kusema anataka kushirikiana na Mataifa mengine ya misaada duniani kuwasaidia watu wa jamii ya Vietnam.
Mfalme huyo wa R&B, hatafnya onyesho lolote la muziki isipokuwa kazi hiyo ya kusaidia jamii pekee na baada ya kumalizaka kwa zoezi hilo atarejea "homeland" kuendelea na michongo yake kama kawa.

IBUA FILMS STAR TANZANIA YAHAMIA MWANZA

Majaji wakishoo love na yale madini yatakayowakilisha jiji la A-town
Baada ya mchakato mzima wa kuibua vipaji vya wasanii chipukizi wa maigizo yaani IBUA Film Star Tanzania kuanzia Arusha,zoezi zima linahamia Mwanza katika Nyanza Shule ya msingi iliyopo Balewa Road tarehe 14 na 15 Novemba kabla ya kuhamia Dodoma.

Chipukizi waliofanikiwa kuiwakilisha mkoa wa Arusha ni pamoja na Salum Ahmed Shafii, Pauline Edward Munisi,Michael Elias Mrema,Mbara Meena na Enhard Haruna. Kutokana na mwamko mkubwa wa wasanii chipukizi,fomu za kujiunga na shindano la IBUA Film Star Tanzania zinaendelea kutolewa maeneo mbali mbali na mikoa husika.Hii ni kuwawezesha wasanii chipukizi kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wao ya kuendeleza vipaji vyao na kuviacha vikipotea kwa kukosa njia ya kuvikuza.

Usaili wa mikoani utaandaliwa vipindi maalum na kuonyeshwa kupitia mojawapo ya runinga hapa nchini.Taasisi ya YEC Production,inayojihusisha na kukuza na kuibua vipaji kwa vijana katika ulingo wa filamu nchini,imegundua njia pekee ya kuibua vipaji hivyo na kuviokoa visipotee kwa kuanzisha shindano maalum la kusaka vipaji.Washiriki wataonyeshwa kwenye runinga kupitia kipindi maalum ambapo watazamaji watahusishwa kumpata staa halisi wa filamu Tanzania.

Mbali na kuviendeleza vipaji vyao pia washiriki watapata mafunzo katika nyanja zote kuanzia za uandishi wa muongozo(scripting)hadi uigizaji bora na kuwawezesha kufikia malengo yao.Vigezo vilivyotumika katika kumsaka msanii huyo chipukizi ni kuwa na umri wa miaka 16 ikiwa ni pamoja na uelewa.

Hata kutokuonekana katika tamthilia au sinema ya aina fulani hapa nchini hicho pia ni kigezo kimojawapo ambacho ni kizuri,kwani vijana wanaochipukia ndiyo wanahitaji msaada mkubwa katika kuibuliwa vipaji,tofauti na wakongwe ambao tayari wamejitangaza.

YEC,imeahidi kuyaangalia matatizo yanayowakabili wasanii kwa kina na kuahidi kutoyarudia, kama yanavyofanywa na baadhi ya wasanii wakongwe,ndiyo maana wameamua kuingia mikataba ya mwaka mmoja na washindi watakaofika kumi bora, ili kuliepuka tatizo hilo.Sambamba na mikataba hiyo kwa watakaofika kumi bora,pia watatoa nafasi ya kuwapeleka shule watakaoingia tano bora kwa ajili ya kujiendeleza mambo mbali mbali ya sanaa ambapo atakayeibuka kinara atapewa zawadi nyingine maalum.

Pia mchakato wa kuwapata washindi kumi hadi tano bora utaanzia kwenye 20 bora, ambapo watacheza filamu mbili huku majaji wakiangalia kipaji cha msanii mmoja baada ya mwingine na kuendelea kuchujwa hadi kupatikana mshindi.

Filamu watakayocheza zitakuwa katika mandhari ya mtanzania halisi,huku asilimia 60 ya mauzo ya kazi hizo yatakayopatikana zitakuwa kwa ajili ya wasanii wenyewe.Kutokana na kuona umuhimu wa suala hilo,Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) liliamua kutoa vibali halali vya kuendesha mchakato huo,ikiwa ni pamoja na kupewa baraka na chama cha hakimiliki Tanzania (COSOTA)ya kusimamia kazi hiyo.Mikoa husika katika mchakato wa kwanza ni Arusha,Mbeya, Zanzibar,Mwanza,Dodoma na Dar es Salaam lakini wigo wa mikoa utaongezeka mwaka hadi mwaka.Jackline WolperBalozi IBUA Film Star Tanzania


NEW FASHION SCARF MUST HAVE

Hapo chacha kina dada scarf hizoooooooooooooooooooooooooooooooo kazi kwetu kuvaa tu.

Elizabeth Go home mumy







Big Brother Revolution Africa Big Brother Revolution Africa


Big Brother Revolution Africa
Sends Elizabeth Home... Elizabeth being show the Door
Fans greet Elizabeth after her eviction last night
-----Tanzania’s Elizabeth was evicted from the BIG BROTHER REVOLUTION during Sunday’s ninth live Eviction Show,leaving just 8 housemates in the running for the massive USD200 000 prize.
After Angolan hip hop star Big Nelo kicked off the show with his hit “Karga”, viewers saw some highlights of the week that was and were given a glimpse of Jeremy’s first day outside the house, it was time to get down to the serious business at hand.IK took the continent inside the house, for Head of House Edward to reveal who he had saved from possible eviction and who he had replaced them with.
Getting straight to the point,Edward told the housemates that he had saved“the only person I get along with,the only person who is cool with me, my little sister Mzamo”.He went on to reveal who he had switched her with:“I changed her with Elizabeth because she took out my twin brother and I miss my brother like nobody’s business”.Big Brother gave Elizabeth 5 minutes to pack her bag and she duly headed upstairs with a few housemates in tow,with Kevin helping her pack her bags.
After a few more inserts,one of which introduced Geraldine’s much-talked-about twin sister Jacqueline to the continent,Big Nelo told viewers he was completely behind Emma before performing another of his hits –“Eu Quero Mais Karga”.IK then called the Alexander Forbes representative on stage to hand over the dreaded envelope and confirm that the name it contained was indeed the correct one.
Having done so, it was time to reveal the news to the housemates and the continent. “The next housemate to leave the Big Brother house is…”said IK.“Elizabeth”.After sharing a long hug with Kevin and greeting the other housemates for the last time,she headed out of the door in the garden and joined IK on stage.Elizabeth revealed that she wasn’t shocked at being evicted because of her role in ending Edward’s twin brother Erastus home.
“Twin power, you know?It’s only a game and you have a good chance of being up for eviction,” she said.“You either get evicted or you win!”IK asked her about the most difficult part of being in the BIG BROTHER REVOLUTION house,to which she replied“I don’t want to say–it’s really personal,but I will say that I’ve learnt a lot about myself in the house and I know my mom is proud of me,” she said.
She felt that her time in the house had taught her to“let things go”and that it was possible to make really good friends in a very short time.IK’s line of questioning then turned to the thing everyone on the continent wanted to know about – her relationship with Kevin.“What’s going on?” he asked her.“Just because I have a man doesn’t mean I have to be mean, said the Tanzanian.“I have a man out there and I put myself in so much danger by getting close to Kevin. Kevin is one of the greatest people I have ever met and he knows things about me that not even my best friends know.”
“Naija boy,I love you!”she shouted.“That’s all I’ll say–he’s my best friend”.Then it was Molotov Cocktail time,with IK promising it was the worst one of the game so far.“It’s a blessing for most and a curse for one,”he read.“All housemates may receive a message from a loved one,except one.”Leaving Elizabeth to make that choice,after a long pause,she named Kevin.“Kevin, I know I’m going to get a message to your loved ones and I know you’ll be there ‘til the end.I’ll deliver a message to your sisters coz you know I have their numbers,”she assured her visibly-upset friend.
Moving on to his final questions,IK asked Elizabeth about the screaming match she had with Itai, in which he had called her“psycho”.“Don’t get into my business if I don’t let you in. It’s mine,” she replied. Asked about her ‘beef’ with Nkenna, Elizabeth declared that it wasn’t a beef and that she just couldn’t relate to the Nigerian.“She tried to be friends with me but it was fake,”she said. After viewing her highlights,IK asked her what she would miss most about the Big Brother house. “I’m gonna miss Kevin,”she told him.
With that,it was time for Elizabeth to depart,with IK reminding her that she left with USD 2809 in her money pot.Here’s how the continent voted: Elizabeth was the least popular in Angola,Botswana,Ghana, Malawi,Namibia,Uganda,Zimbabwe and Zambia.Her fellow nominees Emma and Nkenna were least popular in Ethiopia, Mozambique Nigeria and Rest of Africa and Kenya, South Africa and Tanzania respectively, splitting the vote 8-4-3.

Tuesday, November 3, 2009

Naomba radhi

Jamani naomba radhi kwakutokuonekana oline muda mrefu kwani nilikuwa namatatizo kidogo yaliyo kuwa nje ya uwezo wangu, ninacho wahaidi sasa nimerudi tena hivyo tutakuwa pamoj kuanzia sasa.

Wednesday, September 9, 2009

Jamani hiki ni kipimio cha maco

unatakiwa kubofya katikati palipo namsalaba na kama ikitokea viduara vya pink vinazunguka basi unahitajika kuwahi hospital kwa ajili ya uchunguzi wa mamcho yako kwani inasemekana yatakuwa na kasoro flani.
Picha kwahisani ya www.issamichuzi.blogspot.com

Thursday, August 20, 2009

Vijimambo vyakatuni

he! hii ya kibajaji ni kali kumbe kiki isha mafuta dereva anauwezo wa kukusafirisha kwa njia ya kukibeba ni sawa lakini embu imagine akijikwaa itakuwaje?


sasa wazazi sikuhizi inasemakana wana hadi mabango ya kuozeshea mabinti zao si hatari hii coz kwa yeyote yule atakae leta benk statement we unaye c balaa hili

Friday, August 14, 2009

BREKING NYUUUUZZZZZZZZZ:MADEREVA WA MABASI YA MIKOANI WAGOMA UBUNGO, DAR


MADEREVA WA MABASI YAENDAYO MIKOANI KUTOKEA KITUO KIKUU CHA UBUNGO, DAR, WAMEGOMA KUFANYA KAZI KWA KILE KINACHOSADIKIKA KUWA WANAPINGA HUKUMU YA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA ALICHOPEWA DEREVA MWENZAO ALIYEKUWA ANAFANYA KAZI KATIKA BASI LA MOHAMED TRANS, LILILOPATA AJALI NA KUUA ABIRIA TAKRIBAN 25 SIKU KADHAA ZILIZOPITA,MAENEO YA KOROGWE MKOANI TANGA.
BASI HILO LA MOHAMED TRANS LILILOKUWA LIKITOKEA MWANZA KUJA DAR,LILIGONGANA USO KWA USO NA LORI LA MIZIGO .
HIVI TUNAVYOONGEA HAKUNA BASI LILILOONDOKA UBUNGO TOKEA ALFAJIRI NA ABIRIA WAMEBAKI KURUNDIKANA KILA PEMBE YA KITUO HICHO KIKUU CHA MABASI YA MIKOANI. YAANI NI TAFRANI TUPU.
GLOBU YA JAMII IPO ENEO LA TUKIO NA KAA MKAO WA KULA KWA HABARI NA TASWIRA ZAIDI BAADAYE KIDOOOOOGOOOO..

hashimu ndani ya bongo on tomorrow


mkali wa basketball anatarajia kuwasili ndani ya Dar es salaam hapo kesho.

Tuesday, July 21, 2009

Tuwe makini na hawa wanyama

Haya chacha na yeye kachukia angalia kivumbi chake sijui utambambia nini atulie mtu chali, watu mbio mh! we have to be carefully

Friday, July 10, 2009

ENJOY YOUR WEEKEND

Jamani nawatakia weekend njema najua mambo ya full shangwe ni kawaida ndo maana nimewawekea Remix ya full shangwe ya HUssein machozi tuburudike kabla ya kutembelea sehemu za starehe kwanza.

Enjoy your weekend.

Thursday, July 9, 2009

Msichana mfupi kuliko wote Duniani

Jyoti akiwa na marafiki zake wa shule.
Jyoti akiwa masomoni darasani.


Joyti akiwa na mtoto wa ndugu yake wa umri wa mwaka mmoja.

JOyti akiwa anajisomea




JOyti akiwa darasani

Joyti akiwa amebebwa na wazazi wake.
anaitwa joyti jamani siyo joti, Jyoti Amge wa nchini India ndiye msichana mfupi kuliko wote duniani pamoja na kuwa na umri wa miaka 15 ana urefu wa sentimeta 38 tu na tangia amezaliwa ameongezeka kilo nne tu na kutokana na ufupi wake hata mtoto wa mwaka mmoja anaonekana mkubwa zaidi yake. habari zaidi unaweza ukatembelea

Wednesday, July 8, 2009

Mfalme mpya wa tenisi duniani

Mchumba wa Roger Federer, Miroslava Vavrinec(wa mbele) na mke wa Roddick, Brooklyn Decker wakishuhudia sweet hearts wao wakipambana.
Ni mpambano wa fainali za Wimbledon 2009, Roger Federer Vs Andy Roddick

Federer na mpinzani wake, Andy Roddick


Federer, we acha tu



Aliyekuwa mfalme wa tenisi duniani, Peter Sampras akitoa alama ya kukabidhi ufalme kwa Roger federer baada ya fainali za Wimbledon.




Mfalme mpya wa Tenisi duniani, Roger Federer akibusu kombe.







Federer akishangilia ushindi dhidi ya Roddick
Federer ametwaa kombe la Wimbledon kwa mara ya SITA, na ni mara ya 15 anatwaa makombe makubwa ya tenisi.
Sampras ametwa mataji saba ya Wimbledon, na 14 ya kimataifa.




Siku ya kumuaga mfalme wa pop duniani

Familia ya Michael Jackson kwenye shughuli ya jana
haya chacha mama na t-shirt

Dada wa Michael Jackson,Janet na Latoya wakimfariji mtoto wa Michael, Paris



Jeneza lenye mwili wa Michael Jackson linalo sadikiwa kugharimu dola 25,000 za kimarekani


Kaka wa Michael, Marlon akizungumza kwenye shughuli ya jana, uchungu ulisababisha ashindwe kuendelea.




Enzi za uhai wa king wako jacko.













picha juu king of pop akiwa na watoto wake enzi za uhai wake.






Mtoto wa kwanza wa Michael, Prince akiwa na dada yake, Paris katika shughuli ya kumuaga baba yao jana jijini Los Angeles.








Michael Jackson enzi hizo.









Ndugu wa Michael wakimfariji Paris baada ya mtoto huyo kuwatangazia mamilioni ya watu kote duniani upekee wa baba yake na namna anavyompenda.
Kauli ya mtoto huyo ilisababisha watu wengi wabubujikwe machozi, dah inatia uchungu.











Ndugu wa Michael wakiwamo wasanii wa The Jackson Five wakibeba jeneza lenye mwili wa Michael Jackson jana.










Wanamlilia Michael












Umati uliofika ukumbini jana jijini Los Angeles kumuaga Michael. Watu 20,000 walikuwa ukumbini humo.

SIJAWAHI kushuhudia mtu akiagwa kama Michael Jackson na sidhani kama nitaweza kuona tena hali kama hiyo katika siku za uhai wangu.
Kwa ambaye hakuwa anafahamu nafasi ya Michael katika jamii, yaliyotokea na kusemwa jana yalitosha kumfahamisha hilo, Michael was SPECIAL na hakuna wa kumfananisha naye.
Michael ameaga dunia lakini muziki wake na maisha yake kwa ujumla vitasababisha aendelee kuishi leo na kizazi kijacho.
Dunia imewahi kuwa na wanamuziki wengi, lakini haijawahi kuwa na mtu mwenye karama kama Michael Jackson, anayebisha hajui asemalo.
Alikuwa mwanadamu kama mimi na wewe, alikuwa na udhaifu kama tulionao mimi na wewe, lakini kamwe hatuwezi kujilinganisha naye, he was the biggest star on earth!
Alikuwa na nguvu, si tu za kifedha au kisanii, alikuwa na mvuto wa kipekee kulinganisha wanamuziki wote unaowafahamu.
Michael was the greatest ENTERTAINER on earth, Michael was the greatest STAR earth, kwa wanawe, Michael was the GREATEST father ever!
Buriani Michael, pumzika kwa amani, Amen.